Posts

THAMANI YA KITU ULICHO NACHO

Image
KAMA HUONI THAMANI YA ULICHO NACHO, WENZAKO WANAKITAMANI Kuna watu wana vitu vyenye thamani lakini wanavichezea tu. Hawajui kwamba kuna wengine wanavitamani. Wanatamani vingekuwa vya kwao. Jaribu kufikiri kuhusu nguo. Je, umewahi kununua ama kununuliwa nguo mpya? Angalia jinsi ambavyo nguo mpya inakufanya uanze kudharau nguo zingine zile za zamani. Yawezekana kabisa kuna nguo ulikuwa unaipenda sana kabla hujanunua hii mpya. Lakini mara tu baada ya kununua mpya sasa hivi unaidharau ile ya kwanza, huoni thamani yake. Laiti ungejua kwamba kuna wengine wanatamani hata ile ya zamani waivae hakika usingethubutu hata kidogo kuidharau ile ya kwanza. MAANA YA NENO "THAMANI" Kamusi ya Kiswahili sanifu iliyoandikwa na TUKI na kuchapwa na Oxford, toleo la tatu, inatoa maana ya neno Thamani kuwa ni "Gharama au ubora wa kitu kutokana na hali ya kuhitajika kwake kwenye jamii". Wengine husema "Thamani ni ubora wa kitu kutokana na hali yake na umuhimu wake".  Yesu anasema;...

UMUHIMU WA MACHO YA KIROHO

Image
  UMUHIMU WA MACHO YA KIROHO Na: Mtumishi Frank Mwakapeta BWANA YESU asifiwe… Somo hili limegawanyika katika sehemu zifuatazo; A. Maana ya macho ya kiroho B. Faida za macho ya Kiroho C. Mifano ya watu wenye macho ya kiroho D. Mifano ya watu wasio macho ya kiroho E. Madhara ya kukosa macho ya kiroho F. Mambo ya kufanya ili uwe na macho ya kiroho A. MAANA YA MACHO YA KIROHO Kwa ujumla mwanadamu yeyote anaishi sehemu mbili tofauti; ulimwengu wa mwili na ulimwengu wa roho. Ulimwengu wa mwili ni ulimwengu unaoonekana kwa macho ya nyama (haya mawili ya kawaida). Kwa mfano, macho ya nyama yanaweza kuona kiti, nyumba, mti, gari na ardhi pamoja na vitu vingine vinavyoonekana kwa macho ya kawaida. Ulimwengu wa roho ni ule usioonekana kwa macho ya kawaida. Vitu vya ulimwengu wa roho havionekani kwa macho haya ya kawaida. Kwa mfano, mtu hawezi kumuona mchawi kwa macho ya kawaida, hawezi kuwaona malaika kwa macho ya kawaida. Hawezi kuona nguvu za roho mtakatifu kwa macho ya kawaida. Kwa mantiki...