THAMANI YA KITU ULICHO NACHO
KAMA HUONI THAMANI YA ULICHO NACHO, WENZAKO WANAKITAMANI Kuna watu wana vitu vyenye thamani lakini wanavichezea tu. Hawajui kwamba kuna wengine wanavitamani. Wanatamani vingekuwa vya kwao. Jaribu kufikiri kuhusu nguo. Je, umewahi kununua ama kununuliwa nguo mpya? Angalia jinsi ambavyo nguo mpya inakufanya uanze kudharau nguo zingine zile za zamani. Yawezekana kabisa kuna nguo ulikuwa unaipenda sana kabla hujanunua hii mpya. Lakini mara tu baada ya kununua mpya sasa hivi unaidharau ile ya kwanza, huoni thamani yake. Laiti ungejua kwamba kuna wengine wanatamani hata ile ya zamani waivae hakika usingethubutu hata kidogo kuidharau ile ya kwanza. MAANA YA NENO "THAMANI" Kamusi ya Kiswahili sanifu iliyoandikwa na TUKI na kuchapwa na Oxford, toleo la tatu, inatoa maana ya neno Thamani kuwa ni "Gharama au ubora wa kitu kutokana na hali ya kuhitajika kwake kwenye jamii". Wengine husema "Thamani ni ubora wa kitu kutokana na hali yake na umuhimu wake". Yesu anasema;...